Marehemu Ogolla azikwa nyumbani Alego

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkuu wa majeshi jenerali Francis Ogolla azikwa nyumbani kwake Alego Usonga, kaunti ya siaya akiwa na umri wa miaka 61.

Ogolla alipewa heshima ya risasi 19 wakati wa mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Rais William Ruto.

Maelfu ya waombolezaji walimsifia marehemu Ogolla kuwa msajiri na mwadilifu kwenye utendakazi .

Majeshi ya Kenya yalikabidhi mkewe Ogolla ,Aillen Ogolla bendera ya taifa,bendera ya KDF,viatu na upanga aliokuwa akitumia marehemu.

Jeshi la Kenya litaandaa kumbukumbu Aprili 26 katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex ya kumuenzi.

Marehemu Ogolla alikuwa miongoni mwa wanajeshi 10 waliofariki kwenye mkasa wa ajali ya ndege Ijumaa iliyopita katika kaunti ya Marakwet.

Share This Article