Maraga kuwania Urais mwaka 2027 kwa chama cha UGM

Dismas Otuke
1 Min Read

Jaji Mkuu mstaafu David Maraga atawania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, kwa tiketi ya chama cha United Green Movement (UGM).

Chama cha UGM kilikutana siku ya Alhamisi jijini Nairobi na kuafikiana kwa kauli moja kumteua Maraga kuwa mpepershaji bendera wake katika kinyangányiro cha Urais mwaka 2027.

Maraga alikubali uteuzi huo akiwa tayari kupambana na Rais William Ruto anayewania muhula wa pili afisini.

Alikiri kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais wa sita wa Kenya, lengo lake kuu ni kuhakikisha nchi inaongozwa kwa katiba na sheria zilizopo.

​​

Website |  + posts
Share This Article