Mara Sugar wamejikatia tiketi kwa nusu fainali ya Kombe la Mozzart, kwa mara ya kwanza baada ya kuwalemea Police FC mabao 9-8, kupitia penati, baada ya sare ya bao 1-1, katika muda wa kawaida.
Dennis Cheuruiyot aliwaweka Mara uongonzini kunako dakika ya 11 kabla ya Police kusawazisha kupitia kwa Brian Okoth dakika ya 30.
Ushinde huo umezima matumaini ya maafande kuhifadhi taji hiyo na pia kunyakua mataji mawili msimu huu.
Mara watamenyana na Nairobi United, kwenye nusu fainali huku Gor Mahia, wakiwa na miadi dhidi ya Muranga Seal katika semi fainali ya pili.
Mshindi wa kombe hilo atapokea kitita cha pesa na tiketi ya kuiwakilisha Kenya kwa mashindano ya kombe la Shirikisho msimu ujao.