Miamba wa soka Tanzania bara Simba Sports Club, waliambulia kicha mabao 2-0 na wenyeji RS Berkane ya Morocco katika duru ya kwanza ya fainali ya kuwania kombe la shirikisho la soka Afrika iliyopigwa Jumamosi usiku .
Mamadou Camara, na Oussama Lamlioui, walipachika magaoli ya haraka dakika ya 8 na 14 na kuwaacha Simba na mlima wa kukwea katika mkondo wa pili utakaosakatwa Mei 25 katika uchanjaa wa Amaan jijini Dares Salaam.
Mshindi wa jumla atatwaa kombe la shirikisho na dola za Kimarekani 2,000,000, huku atakayeshindwa akiondoka na dola 1,000,000.