Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kupiga Kura
Samia amewaasa wananchi dhidi ya kutojiandikisha kuwa mpiga kura ni kukosa uzalendo na kujinyima fursa ya kuchagua viongozi chaguo lao.
Rais Samia aliyasema hayo jana Jumamosi baada ya kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Kata ya Chamwino, Jijini Dodoma, ambapo pia ameongea na Wananchi waliokusanyika kwenye kituo cha uandikishaji.
“Niwaombeni sana Wananchi wenzangu tuje kwa wingi tupige kura, huu ni mzunguko wa pili waambieni pia ambao hawajaja, mzunguko wa kwanza umepita tuko kwenye mzunguko wa pili tukikosa mzunguko wa pili mwezi huu na ujao huko mbele hatuna tena nafasi ya kurudia, kwahiyo ili usipoteze haki yako niombe Wananchi wote wawahi kwenye mzunguko huu wa pili, ili twende tujiandikishe tupate haki ya kupiga kura, turudishe Serikali inayoleta maendeleo kwa nchi irudi madarakani”
Tanzania imeratibiwa kuelekea kwenye debe katika uchaguzi mkuu ambapo umepangwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi Oktoba mwaka huu huku Rais Samia akitetea kiti hicho kw atiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM).