Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu fedha Kimani Kuria ametupilia mbali mapendekezo kadhaa tata kutoka kwa Mswada wa Fedha wa 2024.
Tangazo hilo lilitolewa baada ya mkutano wa wabunge wa muungano tawala wa Kenya Kwanza, unaoongozwa na Rais William Ruto, katika Ikulu ya Nairobi.
Miongoni mwa mapendekezo yaliyoondolewa ni mipango ya kutoza asilimia 16 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mkate, huduma za kifedha na miamala ya fedha za kigeni.
Uamuzi huu unafuatia shinikizo endelevu kutoka kwa umma kupitia mitandao ya kijamii kama vile X na tiktok.
Mabadiliko hayo ni pamoja na;
1. Kuondolewa kwa Kodi ya Mkate ya asilimia 16% iliyopendekezwa.
2. Kuondolewa kwa Ushuru wa Bidhaa kwenye mafuta ya mboga umeondolewa.
3. Huduma za Simu: Hakuna ongezeko la ada za miamala kwa huduma za uhamisho wa simu za mkononi; viwango vya sasa vitabakia bila kubadilika.
4. Makato ya Kodi: Makato ya kisheria, kama vile Ushuru wa Nyumba na SHIF, yatakatwa kodi, kupunguza kiasi kinachotegemea PAYE na kuongeza mapato ya matumizi.
5. Ushuru wa Eco: Utatumika tu kwa bidhaa zilizokamilishwa na kuagizwa kukutoka nje. Vitu vinavyotengenezwa nchini, ikiwa ni pamoja na sodo za watoto na sodo zingine hazitazozwa.
6. Kiwango cha VAT: Kimeongezeka kutoka shilingi milioni 5 hadi shilingi milioni 8. Hivi inamaanisha biashara zilizo na mauzo ya chini ya shilingi milioni 8 hazitahitaji kusajili kwa VAT.
7. Msamaha wa eTIMS: Biashara ndogo ndogo zilizo na mauzo ya chini ya shilingi milioni 1 haziruhusiwi kupokea eTIMS.
8. Ushuru wa Bidhaa kwenye Mazao: Ushuru wa Bidhaa unaopendekezwa utatumika kwa mayai, vitunguu na viazi vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, na hivyo kunufaisha wazalishaji wa ndani.
9. Vileo : Ushuru wa bidhaa hizi utatokana na viwango ya pombe. Hii inamaanisha bidhaa zenye viwango vya juu ya pombe nyingi vitatozwa ada zaidi.
10. Michango ya Pensheni: Kiasi kinachoruhusiwa cha michango itakayotozwa ushuru itaongezeka kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 30,000 kila mwezi.
11. Walimu wa Shule za Sekondari za JSS: Fedha zitatengwa kuwaajiri walimu 46,000 wa JSS kuwa wa kudumu na wa kustaafu, na wengine 20,000 wataajiriwa.
12. Kodi ya Magari: Pendekezo la kurekebisha ushuru wa magari kupitia Sheria ya Kodi ya Mapato limetupiliwa mbali ili kuepuka kulemaza sekta ya bima.
13. Usafirishaji wa Miwa: Kodi ya Ongezeko la Thamani katika usafirishaji wa miwa kutoka mashambani hadi viwanda vya kusaga imeondolewa.
Mswada wa Fedha wa 2024 unatazamiwa kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa alasiri ya leo, ukiakisi mabadiliko haya muhimu yanayolenga kuwapunguzia wakenya mzigo wa kifedha.