Maonyesho ya kimataifa ya Nairobi yataanza Jumatatu na kukamilika Oktoba mosi mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri park Showground katika barabara ya Ngong .
Maonyesho ya mwaka huu yamewavutia zaidi ya kampuni 500 kutoka maeneo mbali mbali ulimwenguni zitakazoonyesha na kutangaza bidhaa zao katika sekta za kililo,utengezaji bidhaa,sekta ya nyumba,waekezaji wadogo na wale wa kadri,sekta ya benki,sekta ya umm,sekta ya kibinafsi,sekta ya utalii,elimu na teknolojia .
Ada ya kiingilio kwa watu wazima ni shilingi 300 na shilingi 250 kwa watoto.