Mamake John Pombe Magufuli afariki

Mama Suzana Magufuli, alifariki Jumatatu eneo la Chato, mkoani Geita, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Suzana Magufuli, amefariki dunia.

Mama Suzana Magufuli, alifariki Jumatatu eneo la Chato, mkoani Geita, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kifo cha Suzana kilithibitishwa na mjukuu wake ambaye pia ni mbunge, Jesca Magufuli.

Kifo cha mama Suzana kinajiri takriban miaka mitano baada ya kifo cha mwanawe, ambaye alikuwa Rais wa tano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Share This Article