Mali yasitisha utoaji wa viza kwa raia wa Ufaransa

BBC
By
BBC
1 Min Read

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali imesema nchi hiyo imesitisha utaoji wa vyeti vya usafiri kwa raia wa Ufaransa kwenye ubalozi wake jijini Paris.

Kwenye taarifa, nchi hiyo inasema hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Ufaransa wa kutangaza kuwa Mali ni eneo hatari kutokana na hali ya wasiwasi nchini humo.

Mapema wiki hii, Ufaransa ilisitisha utoaji wa vyeti vya usafiri kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako.

Hali hiyo inasemekana kutokana na kupinduliwa kwa serikali ya Niger na wanajeshi wa nchi hiyo na kuondolewa mamlakani kwa rais aliyechaguliwa Mohamed Bazoum wiki mbili zilizopita.

Serikali za kijeshi za Mali, Burkina Faso, na Guinea ziliapa kuunga mkono utawala wa kijeshi nchini Niger.

Mwaka uliopita, Ufaransa iliwaondoa wanajeshi wake nchini humo baada ya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo kuwaleta mamluki kutoka Urusi.

BBC
+ posts
Share This Article