Makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza hueda yakafikiwa wiki hii, asema afisa wa Marekani

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya South China Monitoring Post

Pande za Israel na kundi la Kiislamu la Hamas huenda zikafikia makubaliano ya kusitisha mapigano wiki hii. 

Makubaliano hayo pia yatahusisha kuachiliwa kwa mateka.

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan anasema makubaliano hayo yanakaribiwa kufikiwa na “yanaweza yakafikiwa wiki hii”.

Sullivan anasema watafanya kila wawezalo kuhakikisha makubaliano hayo yanafikiwa.

Ripoti za vyombo vya habari zinaashiria kuwa Qatar jana Jumatatu iliipatia Israel na Hamas rasimu ya mwisho ya makubaliano hayo.

Qatar ni mpatanishi wa mazungumzo yanayokusudia kusitisha mapigano katika eneo la Gaza.

Waziri mmoja wa Israel ameripotiwa akikariri kuwa Israel inapaswa kuendelea na mashambulizi yake kwa lengo la kuliangamiza kundi la Hamas katika eneo la Gaza.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa Hamas italipa gharama kubwa ikiwa haitawaachilia mateka kabla ya kuapishwa kwake.

Trump ataapishwa Januari 20.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *