Mahakama yazuia Mkutano Mkuu wa Police SACCO ulioratibiwa Jumanne

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama Kuu imezuia mkutano mkuu wa kila mwaka AGM wa chama akiba na mikopo cha Police SACCO ulioratibiwa kuandaliwa kesho Novemba 19, kutokana na malalamishi yaliyowasilishwa mahakamani na baadhi ya wanachama.

Jaji wa mahakama ya viwandani ya Milimani Josephine Mong’are amataja kesi za Utumishi Investment Limited , Ruaraka Housing Estate Ltd na Kenya National Police DT Sacco kuwa za dharura na kuzuia kuandaliwa kwa mikuatno ya AGM hadi pale  kesi hizo zitakapoamuliwa.

Wanachama hao wa Utumishi Investiment Limited iliyo chini ya Police Sacco wanadai kuwa mikutano ya AGM imekuwa ikiitishwa kisirisiri.

Vyama hivyo vya akiba na mikopo vilinuia kuandaa mikutano yao ya AGM kufikia Disemba 31 mwaka huu.

Share This Article