Mahakama yaruhusu kuendelea kwa matozo ya nyumba

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali itaendelea kutekeleza matozo ya nyumba katika mwezi kusubiri uamuzi wa kesi Januari 26.

Hii ni kufuatia uamuzi wa jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa.

Katika uamuzi uliotolewa Januari 3 mwaka huu, majaji wa mahakama ya rufaa Lydia Achode, John Mativo na Mwaniki Gachoka walikubaliana na ombi la serikali kuwa kusitishwa kwa matozo hayo kutalemaza shughuli za serikali.

Mahakama Kuu katika uamuzi wa kesi mnamo Novemba 28 mwaka jana, ilisema matozo ya nyumba yalikuwa kinyume cha sheria.

 

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article