Mahakama Kuu imekataa kusimamisha mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, kufuatilia kesi iliyowasilishwa na michael Onyango Otieno.
Onyango alikuwa amewasilisha kesi mahakamni kupinga mazishi ya Raila, ambayo yanapaswa kufanyika ndani ya saa 72 baada ya kifo chake.
Akitupilia mbali kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Chacha Mwita alisema Onyango alishindwa kubainisha ikiwa mazishi ya Raila yanaandaliwa kinyume na wasia wake.
“Baada ya kusikiliza mawasilisho yake, sijaridhishwa na swala hili la dharura. Mwasilishaji wa kesi hii ameshindwa kubainisha iwapo mazishi ya marehemu yanaandaliwa kinyume na wasia wake ili kutoa fursa kwa mahakama kuchukua hatua,” alisema Jaji Mwita.
Onyango alisema kuwa mazishi hayo yanakiuka sehemu ya 44 ya katiba ya Kenya, inatoa haki kwa mtu kushiriki kikamilifu kwa utamaduni wa jamii yake.
Alidokeza kuwa Raila Odinga alikuwa mfuasi sugu wa utamaduni wa jamii ya Luo.
Raila Odinga alifariki Jumatano asubuhi akipokea matibabu nchini India. Atazikwa Jumapili nyumbani kwake Bondo kaunti ya Siaya.