Mahakama kuu yasema ada ya nyumba ni halali

Marion Bosire
1 Min Read

Mahakama kuu imeamua kwamba ada ya nyumba ilitekelezwa ipasavyo kulingana na katiba na kwamba kulikuwa na ushirikishaji mwafaka wa umma kabla ya kupitisha ada hiyo.

Mwezi Julai mwaka huu, mahakama hiyo ilikosa kutoa agizo la kuharamisha sehemu za sheria ya nyumba za gharama nafuu pamoja na kusitisha makato ya ada ya nyumba.

Jopo la majaji watatu lililokuwa likishughulikia kesi hiyo wakati huo lilisema kwamba sheria zilizopitishwa bungeni huchukuliwa kuwa sawa kikatiba.

Mahakama hiyo ilisema inaweza tu kuingilia iwapo itadhibitishwa kwamba sheria kama hizo zinakiuka katiba ya Kenya.

Jumla ya kesi sita ziliwasilishwa mahakamani kupinga sehemu mbali mbali za sheria ya nyumba za gharama nafuu na baadaye zikajumuishwa na jaji mkuu akateua jopo la kuzishughulikia.

Leo jopo hilo lilitoa uamuzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, kwamba sheria hiyo iko sawa na itaendelea kutekelezwa.

Website |  + posts
Share This Article