Mageuzi yaliyopendekezwa katika NPS, PS na NYS kugharimu bilioni 108

Marion Bosire
1 Min Read

Katibu wa usalama wa ndani Daktari Raymond Omollo amesema kwamba mageuzi yaliyopendekezwa katika huduma ya taifa ya polisi NPS, huduma ya magereza PS na huduma ya vijana kwa taifa NYS yatagharimu shilingi bilioni 108.

Akizungumza katika kikao na washirika wa maendeleo leo, Omollo alisema kwamba mageuzi hayo yanayolenga kuboresha utoaji huduma katika vitengo hivyo vya kiusalama, yatatekelezwa katika muda wa miaka minne, 2024 hadi 2028.

Omollo alisisitiza haja ya juhudi za pamoja, kusasisha washirika kuhusumaendeleo na mfumo wa kimkakati wa kutekeleza mageuzi yaliyopendekezwa na kikosi kazi kilichokuwa kikiongozwa na jaji mkuu mstaafu David Maraga.

Kwa upande wake katibu wa huduma za magereza Daktari Salome Beacco aliangazia haja ya msaada wa kimsingi katika kuboresha miundomsingi, iliyotambuliwa kuwa changamoto kubwa kwenye ripoti ya jopo la Maraga.

Katika ripoti hiyo, jopo hilo lilisema liligundua kwamba vitengo hivyo vitatu vinakabiliwa na changamoto kadhaa kama ufadhili wa kiwango cha chini, ufisadi, uongozi duni, usimamizi mbaya wa nguvu kazi kati ya nyingine.

Jopo la Maraga lilitoa mapendekezo kadhaa kama vile kuboreshwa kwa mazingira ya kikazi kwa maafisa wa vitengo hivyo, kubadilishwa kwa sare, kuboreshwa kwa mishahara kati ya mengine mengi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *