Magavana waunga mkono utumizi wa ushuru wa nyumba kujenga masoko

Tom Mathinji
1 Min Read

Baraza la Magavana limeunga mkono agizo la Rais William Ruto la kutumiwa kwa ushuru wa nyumba katika ujenzi wa masoko ya kisasa.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ahmed Abdullahi, ambaye pia ni Gavana wa Wajir, alisema Baraza hilo linaumga mkono tafsiri ya ushuru wa mpango wa nyumba za gharama nafuu, kujumuosha pia ujenzi wa miundombinu muhimu inaimarisha maisha.

“Masoko ni miundombinu muhimu na huchamgia kwa ukuaji  wa maeneo yaliyoko,” alisema Abdullahi.

Alisema Magavana walishiriki mazungumzo ya kina na Rais William Ruto Juma lililopita na tulikubaliana kuhusu umuhimu wa kuwa na miradi zaidi za kijamii.

Hatua hiyo ya Magavana inajiri huku Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), ambao umeonya kuwa utumizi wa ushuru wa nyumba katika ujenzi wa masoko ni kinyume na sheria.

Website |  + posts
Share This Article