Madalali wavamia makazi ya mbunge wa Naivasha Jane Kihara

Tom Mathinji
1 Min Read
Mbunge wa Naivasha Jane Kihara.

Madalali wamevamia makzi ya mbunge wa Naivasha Jane kihara na kuchukua gari pamoja na mifugo kadhaa.

Kwenye uvamizi huo uliotekelezwa Alhamisi asubuhi, madalali hao walichukua mbuzi na kondoo 100 wanaomilikiwa na mwana wa kiume wa mbunge huyo, na gari moja la kibinafsi la mbunge huyo kuhusiana na kesi ya uchaguzi wa mwaka 2007 kati ya mbunge huyo na mbunge wa zamani wa Naivasha John Mututho.

Baada ya uvamizi huo, wawakilishi wadi na viongozi wengine wa kaunti ya Nakuru walizuru nyumba ya Kihara, huku wakitaja hatua hiyo kama vitisho vya kisiasa.

Aidha, Kihara alitaja uvamizi huo kuwa uliolengwa kumuadhibu kwa sababu ya kumuunga mkono aliyekuwa Naibu Rais ya  Rigathi Gachagua.

Kihara alisema kuna kesi katika mahakama ya rufaa na alishangaa jinsi madalali hao walipata agizo la mahakama.

“Mbuzi na kondoo hao wanamilikiwa na mwana wangu wa kiume, mimi sina mifugo na hata wengine waliibwa wakati wa uvamizi huo,” alisema Kihara.

Mwakilishi wadi wa Naivasha Mashariki Stanley Karanja, alilaani uvamizi huo akiutaja kinyume cha sheria.

Share This Article