Machogu awaasa walimu wa sekondari dhidi ya kuongeza karo

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amewaonya walimu wa shule za sekondari za umma dhidi ya kuwaongezwa wazazi karo.

Machogu amesema kila mwanafunzi wa sekondari za umma atalipiwa shilingi 17,000 na serikali na wala sio 22,000 zilizopendekezwa na baadhi ya walimu wa shule za upili.

Waziri pia amewaonya walimu wakuu dhidi ya kukatalia vyeti vya wanafunzi wa kidato waliofanya mtihani wa KCSE kutokana na malimbikizi ya karo.

Walimu wakuu wa shule za sekondari za umma walipendekeza kuongezwa karo kutokana na hatua ya serikali kupunguza kiwango cha karo inacholipia kila mwanafunzi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *