Rais Ruto aandaa mkutano wa Baraza la Mawaziri kaunti ya Kakamega

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto leo Jumanne asubuhi ameandaa mkutano wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu Ndogo, kaunti ya Kakamega.

Baada ya mkutano huo,  kiongozi wa taifa anatarajiwa kuzindua wodi ya kuwalaza wagonjwa iliyo na vitanda 90 katika hospitali ya kaunti ndogo ya Emuhaya, kaunti ya Vihiga.

Aidha Rais ataweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika kaunti hiyo ya Vihiga, kabla ya kukagua ujenzi wa barabara ya Shamakhokho – Gisambai.

Kisha Ruto atazuru uwanja wa michezo wa Hamisi unaojengwa kabla ya kuzindua ujenzi wa barabara ya Mago-Lusiwi.

Rais Ruto yuko kwenye ziara ya siku tano katika eneo la magharibi mwa nchi.

Website |  + posts
Share This Article