Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20, itashuka katika uga wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kuchuana na Burundi, katika pambano la kundi C, kuwania tiketi ya kufuzu kwa kipute cha AFCON .
Burundi wanaongoza kundi hilo kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Sudan, katika mechi ya ufunguzi na watajikatia tiketi kwa hatua ya robo fainali endapo wataishinda kenya.
Kenya amaarufu Rising Stars, watakuwa wakipiga mechi ya kwanza kabla ya kuhitimisha ratiba dhidi ya Sudan Septemba 19.
Mabingwa wa kombe hilo watafuzu kwa fainali za AFCON mwakani nchini Ghana.