Mabanati wa Kenya waporomoshwa na Uchina,Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya  taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 iliambulia kichapo cha mabao 3-0,  na Uchina katika mchuano wa ufunguzi wa kundi E,kuwania Kombe la Dunia uliopigwa ugani Mohammed 6 jijini Rabat,Morocco, Jumatatu jioni.

XU Yue aliwaweka  Uchina uongozini katika dakika ya 12 wakiongoza kipindi cha kwanza 1-0.
XU Xiaotang alitanua uongozi kwa magoli ya dakika ya 50 na 53, na kuwapa ushindi wa mabao 3 na alama 3 .
Junior Starlets ya Kenya ni sharti waepuke kushindwa na Marekani katika mchuano wa pili Alhamisi hii ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa raundi ya mwondoano.
Marekani waliikung’uta Samoa mabao 17-0 katika mechi nyingine ya kundi E .
Kenya watafunga ratiba ya mechi za makundi Oktoba 25, dhidi ya limbukeni Samoa.

 

Share This Article