Kenya yapokea msaada wa vifaa vya matibabu vya shilingi milioni 83 kutoka India

Vifaa hivyo vinalenga kuisaidia Kenya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo huku visa vinane vikiripotiwa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Afya ya Kenya siku ya Jumatatu imepokea vifaa vya matibabu vya kima cha shilingi milioni 83.39, kutoka kwa serikali ya India.

Vifaa hivyo vinalenga kuisaidia Kenya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo huku visa vinane vikiripotiwa.

Msaada huo ulijumuisha vifaa vya kujikinga 6,000,mitambo 60 ya kutakasa hewa,barakoa aina ya N95 zipatazo 30,000,mitambo ya kuchukua sampuli 86,000,magauni,vifaa vya kufunika nyuso,gumboots na vipimajoto.

Balozi wa India nchini Kenya Adarsh Swaika, akizungumza baada ya kutoa msaada huo uliopokelewa na katibu wa afya ya umma Mary Muthoni,alisema vifaa hivyo vitatumika na wahudumu wa afya,vituo vya kuwatengea wagonjwa,watoa huduma ya dharura katika maeneo ya kuingia nchini Kenya na vituo vya afya.

Serikali ya Kenya ilikariri kujitolea kukabiliana na maambukizo ya ugonjwa wa Ebola.

Share This Article