Maafisa wapya wa KECOSO wachaguliwa bila kupingwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa watatu wa chama cha michezo ya mashirika ya mawasiliano nchini(KECOSO), walichaguliwa bila kupingwa katika mkutano mkuu wa mwaka ulioandaliwa Jumanne katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Maafisa waliochaguliwa bila upinzani na ambao watahudumu kwa kipindi cha miaka minne ni pamoja na mwenyekiti wa kamati andalizi ya michezo ya KECOSO Ben Juma,msimamizi wa vipindi vya Radio katika shirika la KBC Omole Asiko akachaguliwa katibu mkuu hUku Philip Kipkagat akichaguliwa mtunza hazina.

Mkutano huo ulisimamiwa na msajili wa michezo nchini Rose Wasike na kuhudhuriwa na wanachama wengine kutoka kwa Baraza la Michezo nchini akiwemo naibu Rais wa Shirikisho la Voliboli nchini Paul Bitok, aliyewasilisha mashirikisho ya michezo.

Zaidi ya wachezaji 3,000 wanatarajiwa kukongamana katika jiji la Nakuru mwezi Agosti mwaka huu kwa makala ya 43 ya michezo ya KECOSO.

TAGGED:
Share This Article