Maafisa wa polisi waandaa mkutano wa injili mjini Meru

Marion Bosire
1 Min Read

Maafisa wa polisi kutoka sehemu mbali mbali nchini waliandaa mkutano wa injili mjini Meru, hatua iliyogusa wakazi wa eneo hilo.

Mtindo wa kuhuburi wa maafisa hao wa usalama ulivutia wengi mjini huko wakakusanyika kuwasikiliza.

Mchungaji Martin Wanjala ambaye ni afisa wa polisi, anasema uamuzi wa kuandaa mkutano wa injili mjini Meru ulilenga kuleta watu pamoja waishi kwa amani hasa wakati huu ambapo gharama ya maisha imepanda na muungano wa Azimio la Umoja umeitisha maandamano.

Wanjala alisema wananchi huchukulia maafisa wa polisi kuwa wenye kiburi na wasioamini neno la Mungu, ndiposa wakaamua kuandaa mikutano ya injili katika sehemu mbali mbali kuhamasisha umma.

Alisihi wakenya waishi pamoja kwa amani na upendo bila kijali kabila kwani sote ni wanakenya.

Mchungaji John Gikunda wa kanisa la PEFA mjini Meru alipongeza maafisa hao wa polisi kwa hatua waliyochukua akisema ni ya maana katika kusaidia wakenya kuwa na imani nao na kuwasaidia wanapotekeleza kazi yao ya kudumisha usalama.

Ripoti yake Jeff Mwangi

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *