Maafisa 208 wa polisi wa Kenya warejea kutoka Haiti

Tom Mathinji
1 Min Read

Kikosi cha tatu cha maafisa wa polisi wa Kenya kimerejea hapa nchini kutoka Haiti, walikotumwa kudumisha amani chini ya Kikosi cha kimataifa cha maafisa wa usalama (MSS).

Maafisa hao 208, walitua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumanne jioni.

Walipowalisi, walilakiwa na mshauri wa serikali kuhusu maswala ya usalama Monica Juma, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, pamoja na maafisa wengine wakuu wa polisi.

Akizungumza alipowapokea maafisa hao, Juma aliwapongeza kwa utaalam na kujitolea kwao na maadili akidokeza  kuwa huduma yao imeletea taifa hili sifa njema.

Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja, aliwapongeza maafisa hao kwa kudumisha nidhamu akiwahakikisha kuunga mkono maslahi ya maafisa hao , ikiwa ni pamoja afya ya akili huduma za ushauri nasaha.

Kulingana na Huduma ya Taifa ya Polisi, kikosi hicho kimesaidia kushikilia vifaa muhimu nchini Haiti kama vile viwanja vya ndege, bandari na njia muhimu za uchukuzi hatua iliyofanikisha uchukuzi wa wananchi na utoaji wa huduma za kibinadamu.

Share This Article