Mbunge Peter Salasya atakiwa kufika mbele ya NCIC

Tom Mathinji
1 Min Read
Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya.

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya, anatarajiwa kufika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Mshikamano na Utangamano (NCIC) Jumanne,kuhusiana na matamshi yanayodaiwa kuwa ya ubaguzi wa kikabila.

Kulingana na tume hiyo, Salasya anakabiliwa na kesi ya kuchochea ukabila na anatarajiwa kuhojiwa na maafisa wake Jumanne asubuhi.

Salasya, alifunguliwa mashtaka Mei 19, 2025 katika mahakama moja ya Nairobi kwa kudaiwa kutoa semi za chuki.

NCIC imemshtumu mbunge huyo kwa kuchochea uhasama kati ya jamii ya Luo na Luhya, kupitia ujumbe kwenye ukurasa wake wa X mnamo Mei 10, 2025.

Mbunge huyo anadaiwa kuchapisha ujumbe huo,akifahamu ni wa kukejeli, kuchoea na kuibua chuki kati ya jamii hizo mbili.

Kosa hilo linakiuka sehemu ya 13(1)(b) na 13(2) ya sheria za Tume ya kitaifa ya Mshikamano na Utangamano ya mwaka 2008.

Tume hiyo imetoa tahadhari kuhusu joto la kisiasa hapa nchini, huku semi za chuki na uchochezi zikiongezeka.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article