Lissu achaguliwa makamu mwenyekiti wa IDU

Lissu alichaguliwa katika uchaguzi wa viongozi wapya uliofanyika mwisho wa mikutano ya muungano huo nchini Ubelgiji.

Marion Bosire
2 Min Read
Tundu Lissu, Kiongozi CHADEMA

Mwanasiasa wa Tanzania Tundu Lissu amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa muungano wa vyama vya kidemokrasia duniani -IDU.

Lissu ambaye ni mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA na ambaye amezuiliwa nchini Tanzania kwa kile kinachodaiwa kuwa uhaini alichaguliwa mwisho wa mkikutano ya muungano huo Jijini Brussels, nchini Ubelgiji.

CHADEMA ilisema katika taarifa kwamba chama hicho kiliwakilishwa kwenye mkutano huo na Deogratias Munishi ambaye ni katibu mkuu wa baraza la kitaifa la vijana la CHADEMA.

Munishi anahudumu pia kama makamu mwenyekiti wamuungano wa demokrasia barani Afrika  Democracy Union of Africa – DUA  Kanda ya Afrika Mashariki.

Wajumbe wa muungano huo wa International Democracy Union – IDU  walimchagua pia aliyekuwa waziri mkuu wa Canada Stephen J Harper kuendelea kuwa mwenyekiti kwa miaka mitatu ijayo.

Lissu alichaguliwa pia kuwa sehemu ya jopo la makamu wenyeviti wa DUA hatua ambayo CHADEMA inahusisha na rekodi ya msimamo wake usioyumba katika kupigania haki, utawala bora na demokrasia nchini Tanzania.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alisifiwa kwamba hata ingawa mazingira ni hatarishi ambapo kumewahi kuwa na jaribio la kumtoa uhai kama ilivyoelezwa kwenye mkutano mkuu wajumbe kutoka Mataifa mbalimbali ulimwenguni walimotishwa kumchagua Lissu kwa wadhifa huo.

Wajumbe wa mkutano mkuu wa IDU walisema pia kwamba kwa uzoefu wake katika mapambano ya kutafuta demokrasia ya kweli, haki na uhuru wa kweli, Lissu atatoa mchango mkubwa ndani ya IDU.

Walitaja jukumu la kumulika maeneo yanayokabiliwa na changamoto za kuporomoka au kudorora kwa demokrasia na kuibuka kwa tawala za kiimla husani bara la Afrika.

Website |  + posts
Share This Article