Lebanon: Mashambulizi ya Israel yasababisha vifo vya watu 51

Tom Mathinji
1 Min Read

Mashambulizi ya Israel huko Lebanon leo Jumatano, yamesababisha vifo vya watu 51, huku zaidi ya 220 wakijeruhiwa, haya ni kwa mujibu wa waziri wa Afya wa Lebanon Dkt. Firass Abiad.

Jeshi la ulinzi la Israel IDF, limesema limefanikiwa kushambulia mamia ya maficho ya kundi la Hezbollah, likishtumu kundi hilo kwa kuficha silaha katika makazi ya raia.

Kulingana na ripoti za jeshi hilo, maeneo 280 ya Hezbollah yameshambuliwa na ndege za kivita za Israel.

Wakati uo huo hospitali nchini Lebanon zinaripotiwa kuzidiwa baada ya mashambulizi ya wiki jana.

Dkt. Tania Baban, mkurugenzi wa huduma za misaada ya matibabu, MedGlobal Lebanon, alionyesha wasiwasi kwamba mfumo wa huduma ya afya nchini humo umedororra na unaweza kuporomoka kabisa.

Kwa upande mwingine shirika la Umoja wa Mataifa, limesema kuwa takriban watu 60,000 Kaskazini mwa Israel, wamehamishwa makwao kutokana na mashambulizi ya kila siku ya kundi la Hezbollah

TAGGED:
Share This Article