KWS yathibitisha kutokuwepo kwa simba Langata

Tom Mathinji
1 Min Read
Wakazi wa Lang'ata walidai kuwaona Simba katika eneo hilo.

Shirika la huduma kwa wanyamapori (KWS), limethibitisha kuwa halijapata simba katika eneo la Langata kama ilivyodaiwa na wakazi.

Shirika hilo limethibitisha hayo leo Alhamisi kupitia ujumbe kwenye mtandao wa X, baada ya ripoti Jumatano jioni kudai kwamba simba walionekana karibu na gereza la wanawake eneo la Langata jijini Nairobi.

Kulingana na shirika hilo, baada ya kupokea ripoti hiyo, lilituma kikosi chake kusaka simba hao usiku kucha lakini hawakupata simba yeyote.

“Kikosi cha Kudhibiti Wanyama cha KWS kilitumwa mara moja kufanya msako wa kina katika eneo hilo usiku kucha. Licha ya juhudi zao, hakuna simba waliopatikana,” KWS ilisema kwenye taarifa.

Hata hivyo, kikosi hicho kinafuatilia hali hiyo kwa karibu na kiko katika tahadhari kubwa.

Aidha, liliwataka wakazi kukaa macho na kuripoti tukio lolote la wanyamapori kwa nambari ya simu ya KWS ya saa 24 ya 0800 597 000 au WhatsApp 0726 610509, ili kuingilia kati mara moja.

KWS liliwahakikishia Wakenya kuwa linaweka kipaumbele usalama wa umma wakati wowote ule.

TAGGED:
Share This Article