KUCCPS yafungua tovuti kwa ajili ya uhamisho kati ya taasisi

Rahab Moraa
1 Min Read

Huduma ya kutoa nafasi kwa wanafunzi katika vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu nchini, KUCCPS imefungua tovuti yake kwa ajili ya maombi ya uhamisho baina ya taasisi kwa mwaka wa 2024.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, KUCCPS iliagiza wanafunzi waliowekwa katika vyuo vikuu na taasisi tofauti nchini mwezi uliopita (Mei 2024) wanaotaka kubadilisha taasisi kutuma maombi kupitia kiungo cha http://students.kuccps.net.

KUCCPS katika tangazo lake ilisema kuwa mchakato huo pia utaruhusu mabadiliko ya kozi kulingana na waombaji kukutana na alama za kupunguzwa.

Waombaji watakuwa na siku 30 kufanya mabadiliko wanayopendelea baada ya hapo tovuti itafungwa mnamo Julai 4, 2024.

Ili mtu astahiki uhamisho, mwombaji lazima awe amewekwa katika programu anayotafuta uhamisho kutoka.

Tangazo hilo la KUCCPS linajiri siku moja baada ya kamati ya Bunge ya Elimu kuagiza Wizara ya Elimu kuondoa barua zote za kujiunga na chuo kikuu.

Rahab Moraa
+ posts
TAGGED:
Share This Article