Inspekta Mkuu wa Polisi atakiwa kutoa ushahidi wa kukodiwa kwa miili

Dismas Otuke
1 Min Read

Wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti kote nchini wamemtaka Inspekta Mkuu wa Polisi Japhet Koome kutoa ushahidi wa miili iliyokodiwa na wanasiasa wa upinzani kutoka kwenye vyumba hivyo wakati wa maandamano na kudai kuwa waliofariki walikuwa waathiriwa wa ukatili wa polisi. 

Wahudumu hao wametaja kauli ya Koome kuwa kejeli kwa familia zilizopteza wapendwa wao wakati wa maandamano yaliyoitishwa na muungano wa Azimio wiki chache zilizopita.

Chama cha wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti nchini kimemtaka Koome kutoa ushahidi kuthibitisha kauli zake.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari akiwa katika chuo cha makurutu wa polisi huko Kiganjo, Nyeri jana Jumatano, Koome alidai kuwa viongozi wa upinzani walikodi miili kutoka kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti na kisha kuwanyoshea maafisa wa polisi kidole cha lawama kwa madai kuwa ni wao waliowaua waliofariki.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amepuuzilia mbali matamshi hayo akiyataja kuwa yasiyokuwa ya kweli.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *