Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema walimu wanostaafu watakuwa wakipokea malipo ya uzeeni ndani ya miezi sita baada ya kustaafu.
Akijibu swali la seneta wa Embu Alexander Maundigi, Machogu amesema mwajiri anapaswa kuwasilisha stakabadhi na arifa ya kustaafu kwa walimu huku mchakato wote kufikia malipo ukifanywa ndani ya miezi mitano hadi sita.
Takriban walimu 24,000 waliostaafu kufikia mwaka 1998 hawajapokea malipo yao ya uzeeni kufikia sasa.