Maandalizi yamepamba moto kabla ya kuandaliwa kwa Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji la Nyanza ambalo linakusudia kuchechemua ustawi wa eneo hilo.
Kongamano hilo la siku mbili litaandaliwa kati ya Februari 6-8 mwaka huu jijini Kisumu.
Maudhui ya kongamano hilo litakaloandaliwa katika hoteli ya Ciala ni, “Nyanza yainuka – Kuelekea Mabadiliko ya Kiuchumi kwa ajili ya Ukuaji na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.”
Viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.
Rais William Ruto atahudhuria kama mgeni wa heshima huku Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga akialikwa kama mgeni maalum.
Mawaziri na Mgavana ni miongoni mwa viongozi ambapo pia watahudhuria.