Kocha Firat awaita wanandinga 28 kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026

Dismas Otuke
2 Min Read

Kocha wa Timu ya Haifa ya Kenya, Harambee Stars Engin Firat,ametaja kikosi cha wanandinga 28 ,watakaowajibika katika mechi mbili za baadaye mwezi huu kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2026 dhidi ya Gabon na Ushelisheli mtawalia.

Kikosi hicho kinawajumuisha wachezaji wa kulipwa na wale wa humu nchini, huku Nabi Kibunguchy Orlando City ya Marekani na Eric Balecho wa Murang’a Seal na Hanif Wesonga wa KCB wakiitwa kwa mara ya kwanza timuni.

Wachezaji Duncan Otieno wa Gaborone United ya Botswana ,Timothy Ouma wa Elfsborg ya Uswidi na Eric Johanna wa UTA ARAD ya Uhispania wamerejeshwa kikosini.

Harambee Stars watafungua mechi za kundi F, kufuzu kombe la dunia ugenini tarehe 16 mwezi huu dhidi ya Gabon mjini Franceville, kabla ya kuchuana na Ushelisheli siku nne baadye mjini Abidjan Ivory Coast.

Wachezaji wa kigeni watarajiwa kuwasili nchini kuanzia Ijumaa usiku, huku kikosi hicho kikisafiri kwenda Gabon Novemba 15 .

Kenya imo kundi F la kufuzu kwa fainali za kombe la dunia pamoja na Côte d’Ivoire, Gabon, Gambia, Burundi, na Ushelisheli.

Kikosi kamili kilichoitwa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwezi huu kinawajumuisha:-

Makipa

Patrick Matasi (Kenya Police), Ian Otieno (Zesco), Joseph Ochuka (Bandari)

Mabeki

Nabi Kibunguchy (Orlando City), Hanif Wesonga (KCB), Abud Omar (Kenya Police), Daniel Sakari (Tusker), Geoffrey Ochieng (Gor Mahia), Daniel Anyembe (Viborg), Eric Ouma (AIK), Joseph Okumu (Reims), Johnstone Omurwa (CF Estrela), Amos Nondi (Ararat)

Kiungo

Duncan Otieno (Gaborone United), Teddy Akumu (Sagan Tosu), Duke Abuya (Singida), Ayub Masika (Nanjing City), Kenneth Muguna (Kenya Police), Eric Balecho (Murang Seal), Rooney Onyango (Gor Mahia), Eric Johanna (UTA ARAD), Richard Odada (Aalborg), Alfred Scriven (Hodd), Timothy Ouma (Elfsborg)

Washambulizi

Masud Juma (Al Faisaly), Michael Olunga (Al Duhail), Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Benson Omalla (Gor Mahia)

Website |  + posts
Share This Article