Kocha wa timu ya taifa ya Soka ya Kenya-Harambee Stars,Engin Firat ametaja kikosi cha wanandinga 24, wakaoshiriki mechi mbili za kundi J kufuzu kwa fainali za kombe la AFCON dhidi Cameroon.
Harambee Stars itachuana na wenyeji Indomitable Lions ya Cameroon katika mkumbo wa kwanza keso kuanzia saa moja usiku, katika uchanjaa wa Ahmadou Ahidjo Omnisports mjini Yaoundekabla ya mechi ya marudio kusakatwa katika kiwara cha Mandela National nchini Uganda.
Nahodha na mshambulizi Michael Olunga anarejea kikosini baada ya kukosa mechi mbili za mwezi uliopita dhidi ya Zimbabwe na Namibia kutokana na jeraha.
Timu hiyo imeondoka nchini mapema leo na inatarajiwa kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza saa moja leo usiku.
Mechi zote mbili za Kenya dhidi ya Cameroon zitarushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.
Makipa
Ian Otieno, Patrick Matasi, Byrne Omondi
Mabeki
Alphonce Omija, Daniel Anyembe , Amos Nondi, Sylvester Owino, Johnstone Omurwa, Collins Sichenje, Joseph Okumu, Geoffrey Ochieng, Eric Ouma
Viungo
Chrispine Erambo, Richard Odada, John Ochieng, Timothy Ouma, Anthony Akumu, Duke Abuya, Ronney Onyango
Washambulizi
John Avire, Michael Olunga, Jonah Ayunga, Adam Wilson, Alfred Scriven
Kenya na Cameroon zinaongoza kundi J kwa pamoja kwa alama 4 kila moja huku Zimbabwe ikiwa ya tatu kwa alama 2 wakati Namibia wakiwa bila alama