Klabu ya Santos aliyoichezea mchezaji nguli marehemu Pele imeteremshwa ngazi kutoka ligi kuu ya Brazil Serie A kwa mara ya kwanza baada ya miaka 111.
Santos imeshushwa ngazi kutoka ligini mapema Alhamisi baada ya kuambulia kichapo cha magoli mawili kwa moja nyumbani dhidi ya Fortaleza.
Santos pamoja na Flamengo na Sau Paulo zilikuwa timu tatu kwenye ligi hiyo, ambazo hazikuwahiteremshwa ngazi.
Marehemu Pele aliichezea Santos baina ya mwaka 1950 na 1960 akiisaidia kutwaa mataji 10 ya Ligi Kuu.
Timu hiyo pia ilitawazwa mabingwa wa bara Amerika Kusini maarufu kama Cope Libertadores mwaka wa 1962 na 1963.
Santos imewatoa wachezaji maarufu kama vile Robinho, Neymar na Rodrigo wa Real Madrid.