Kipyegon na Kipkorir waridhia shaba mbio za barabara duniani

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa dunia katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon na Nicholas Kipkorir, wamenyakua medali za shaba katika makala ya kwanza ya mbio za barabara dunia mjini Riga Latvia siku ya Jumapili.

Kipyegon aliyekuwa akiongoza kutoka mwanzo alizidiwa maarifa katika mita 500 za mwisho za kuchukua nafasi ya tatu  katika mbio za maili moja kwa dakika  4 sekunde 24 nukta 13.

Chipukizi wa Ethiopia Diribe Welteji, ameibuka mshindi akiweka rekodi mpya ya dunia ya dakika 4 sekunde 20 nukta 98 huku mwenzake Freweyni Hailu akishinda fedha.

Nicholas Kipkorir alishinda medalia ya fedha katika mbio za kilomita 5 kwa kutumia dakika 13 na sekunde 16 nyuma ya Wahabeshi Hagos Gebrehiwet na Yomif Kejelcha walionyakua nishani za dhahabu na fedha.

 

Share This Article