Faith Kipyegon atawania kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda dhahabu tatu mtawalia katika fainali ya mita 1,500, atakapojitosa uwanjani Jumamosi usiku kwenye fainali ya shindano hilo.
Kipyegon ambaye alishinda dhahabu ya Olimpiki mwaka 2016 na na kuhifadhi mwaka 2021, anawinda dhahabu hiyo, baada ya kukosa dhahabu ya fainali ya mita 5,000.
Bingwa huyo wa dunia atashiriki fainali hiyo pamoja na mwanariadha wa Kenya mwenye makao yake nchini Marekani Susan Ejore.
Fainali hiyo itaanza saa tatu na robo.