Kipyegon ateuliwa kuwania tuzo ya Laureus

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon ameteuliwa kuwania tuzo ya Laureus ya Mwanaspoti bora wa kike mwaka uliopita.

Ni mwaka wa tatu mtawalia kwa Kipyegon kuteuliwa kuwania tuzo tangu mwaka 2024 huku mshindi akitarajiwa kubainika tarehe 20 mwezi ujao mjini Madrid, Uhispania.

Kipyegon alishinda taji ya nne ya mita 1500 ya Dunia mwaka jana katika mashindano ya Tokyo, akiwa mwanamke wa kwanza kuafikia historia hiyo.

Pia alivunja rekodi ya dunia ya mita 1,500 na pia alishinda mbio za maili moja za Athlos.

Bingwa huyo mara nne wa Dunia atashinda na mabingwa wenza wa dunia Jefferson-Wooden na Sydney McLaughlin-Levrone, wote kutoka Marekani, mchezaji tenisi

Aryna Sabalenka, mwogeleaji Katie Ledecky, na mwanasoka Aitana Bonmati.

Share This Article