Kiptum na Chepng’etich kushiriki Chicago Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa mashindano ya London na Chicago Marathon Kelvin Kiptum na Ruth Chepngetich wamethibitisha kuwa watashiriki makala ya mwaka huu ya mbio za Chicago Marathon zitakazoandaliwa nchini Marekani Oktoba 8.

Kiptum, ambaye ni mwanariadha wa pili mwenye kasi katika marathoni, atapambana na bingwa mtetezi Benson Kipruto, Daniel Mateiko na Wesley Kiptoo watakaoshiriki kwa mara ya kwanza.

Bingwa mtetezi kwa vipusa Ruth Chepngétich atakabiliana na Joyceline Jepkosgei aliye na muda bora wa saa 2, dakika 17 na sekudne 43, pamoja na Stacey Ndiwa na Wahabeshi wanne Genzebe Dibaba, Sutume Kebede, Tigist Girma na Ababel na bingwa wa London Marathon Sifan Hassan kutoka Uholanzi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *