Kindiki awarai vijana kujisajili kuwa wapiga kura

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki awarai vijana kujisajili kuwa wapiga kura.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, ametoa wito kwa waliohitimu kuwa wapiga kura, kujitokeza kwa wingi na kujisajili, ili wapate fursa ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Kindiki alisema mchakato wa usajili wa wapiga kura unaoongozwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, unawapa fursa wakenya waliohitumu haki ya kikatiba ya kushiriki kwa Uchaguzi Mkuu.

“Nawahimiza wote waliohitimu kuwa wapiga kura na bado hawajasajiliwa, kuhakikisha wamesajiliwa kwa kuwa ni haki yao ya kupiga kura,” alisema Naibu huyo wa Rais.

Aliyasema hayo Ijumaa wakati wa zoezi la uhamasishaji wa kiuchumi katika  uwanja wa General Kago,eneo bunge la Kangema kaunti ya Murang’a.

“Taifa hili ni la kidemokrasia na njia ya kuwachagua viongozi ni kupitia uchaguzi. Nawahimiza vijana wajisajili ili wawachague viongozi wanaowataka. Bila kusajiliwa hutapata nafasi ya kushiriki katika maamuzi hayo,” aliongeza Kindiki.

Kulingana na Kindiki, uwanja huo wa General Kago, ambao ulipewa jina hilo baada ya shujaa wa Mau Mau General Kago, utaboreshwa hadi kufikia viwango vya kimataifa.

Website |  + posts
Share This Article