Kila sehemu ya nchi itanufaika na maendeleo, asema Gachagua

Martin Mwanje
1 Min Read

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema serikali ya Kenya imekusudia kutekeleza maendeleo kila pembe ya nchi. 

Anasema kama serikali, wanaendelea kushauriana na kubadilishana mawazo na viongozi kutoka kote nchini kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika Mpango wa serikali wa kutekeleza miradi ya maendeleo kote nchini.

Alisema hayo alipokutana na viongozi kutoka kaunti ya Kisii katika makazi yake rasmi mtaani Karen, wakiongozwa na kiranja wa wengi katika bunge la taifa Sylvanus Osoro.

Mbunge wa Kitutu Chache Kaskazini Japheth Nyakundi na Wawakilishi Wadi pia walihudhuria mkutano huo.

“Hii ni sehemu ya utimizaji wa Mpango wetu ambao unahakikisha kwamba kila sehemu ya nchi inanufaika kutokana na mipango ya maendeleo ya serikali kwa usawa,” alisema Gachagua.

Awali, Naibu Rais alisema serikali ya Kenya Kwanza itatekeleza maendeleo kila sehemu ya nchi bila kujali miegemeo ya kisiasa.

Share This Article