Argentina yaelezea nia ya kujiondoa WHO

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Argentina Javier Milei.

Rais Javier Milei wa Argentina ameelezea nia ya nchi hiyo kujiondoa kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Msemaji wa Rais huyo amesema sababu ya taifa hilo kujiondoa kutoka kwa WHO, ni tofauti za kina kuhusu usimamizi wa masuala ya afya na shirika hilo hasa wakati wa kupambana na janga la Covid-19.

Tangazo la Argentina linajiri wiki mbili baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutia saini agizo la kuanza kujiondoa kwa Marekani kutoka kwa shirika hilo.

Mataifa hayo mawili yamelalamikia jinsi shirika hilo lilivyoshughulikia dharura ya Covid-19, ambapo Argentina ilikumbwa na hali ya kutotoka nje kwa muda mrefu na madai ya ushawishi wa China kwenye shughuli za shirika hilo.

Marekani ni mfadhili mkuu wa WHO ikichangia dola za Marekani milioni 950 mwaka uliopita ikiwa ni asilimia 15 ya bajeti nzima ya shirika hilo, hivyo kujiondoa kwake kutaathiri pakubwa shughuli za shirika hilo.

Argentina kwa upande wake huchangia dola milioni 8 kila mwaka.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article