Kikao cha kumbandua madarakani Naibu Rais chaendelea bungeni

Martin Mwanje
1 Min Read
Mwengi Mutuse - Mbunge wa Kibwezi Magharibi

Bunge la Kitaifa kwa sasa linaandaa kikao cha kumbandua madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua. 

Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse amewasilisha bungeni hoja maalum ya kutaka Gachagua abanduliwe madarakani.

Mutuse amewasilisha mashtaka 11 anayosema ni ushahidi tosha unaodhihirisha Gachagua hapaswi kushikilia wadhifa huo.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni pamoja na kumkosea Rais heshima, kuchochea semi za chuki na kujilimbikizia mali kwa njia za kutilia shaka.

Hoja ya kumbandua Gachagua madarakani imeungwa mkono na jumla ya wabunge 291.

Wabunge kwa sasa wanachangia hoja hiyo na kisha Gachagua atapewa fursa ya kujitetea dhidi ya madai aliyolimbikiziwa kuanzia majira ya saa 11 jioni.

Mbunge wa Rachuonyo Otiende Amollo alikuwa wa kwanza kuchangia hoja hiyo na kutangaza kuwa anaiunga mkono.

 

 

Share This Article