Wanariadha wote watatu wa Kenya Leonard Bett,Abraham Kibiwott na Simon Koech wamefuzu kwa fainali ya mbio za mita mita 3,000 kuruka viunzi na katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha Ulimwenguni mjini Budapest Hungary Jumamosi Adhuhuri.
Bett amemaliza wa tatu katika mchujo wa tatu kwa dakika 8 sekunde 16 nukta 74,mchujo ulioshindwa na Lamecha Girma wa Ethiopia.
Kibiwot lifuzu kwa fainali baada ya kuchukua nafasi ya nne katika mchujo wa pili akitumia dakika 8 sekunde 24 nukta nukta 31, katika mchujo ulioongozwa na Kenth Rooks wa Marekani.
Koech alimaliza wa tatu katika mchujo wa kwanza kwa dakika sekunde 20 nukta 29 na kujikatia tiketi kwa fainali .
Fainali ya shindano hilo itaandaliwa Jumanne ijayo huku Wakenya hao wakipambana na bingwa mtetezi Soufiane El Bakkali wa Morocco.