Kesi ya kutimuliwa kwa Gachagua yaanza kwa wanasheria kukabana koo

Martin Mwanje
1 Min Read

Kusikizwa ya kesi ya kutimuliwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua imeanza kwa wanasheria wa pande zote katika kesi hiyo kutifua kivumbi cha sheria juu ya faili zilizo mbele ya jopo la majaji watatu wanaosikiza kesi hiyo.

Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Eric Ogola, Athony Mrima na Freda Mugambi liliteuliwa na Jaji Mkuu Martha Koome kusikiza kesi hiyo.

Wanasheria wa Gachagua wametilia shaka kubuniwa kwa jopo hilo na kesi zitakazosikizwa katika kesi hiyo.

Gachagua alikuwa amewasilisha kesi zipatazo 20 kupinga kubanduliwa kwake madarakani, kesi ambazo mahakama ilizijumuisha pamoja.

Hususan, wanasheria wa Gachagua walitaka kubaini ikiwa faili ya kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya Kerugoya imewasilishwa mbele ya jopo hilo.

Katika agizo lake, mahakama ya Kerugoya ilizuia kuapishwa kwa Naibu Rais mteule.

Majaji hao waliwataarifu kuwa faili hiyo haijawasilishwa kwao.

Rais William Ruto kupitia wanasheria wake ametaka kesi hiyo kuwasilishwa mbele ya Mahakama ya Juu akisema Mahakama Kuu haina mamlaka ya kuisikiza.

 

Website |  + posts
Share This Article