Serikali yafutilia mbali mawakala bandia wa ajira za ughaibuni

Serikali yafutilia mbali mawakala bandia wa ajira za ughaibuni

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imefutlia mbali mawakala bandia wanaowasajili Wakenya kwa kazi za ughabuni ili kuhakikisha sekta hiyo ina maadili na Wakenya hawatapeliwi.

Katibu katika Wizara ya Leba na ukuzaji maarifa Shadrack Mwadime, amesema haya alipohudhuria ya kufuzu kwa mahafali 24, waliohitimisha mafunzo ya upigaji mbizi katika chuo cha mafunzo ya Ubaharia cha Bandari .

“Ni jukumu letu kama serikali kusafisha sekta hii. Huenda kazi ni nadra kupatikana lakini ajira zipo nyingi ughaibuni.” akasema Mwadime

Mwadime ameongeza kuwa mchakato wa kuondoa mawakala wote bandia katika sajili ya serikali unaendelea hadi kuwe na uadilifu.

Alitoa hakikisho kuwa Wakenya wote waliotapeliwa na mawakala hao bandia watarejeshewa pesa zao na wahusika wachukuliwe adhabu za kisheria.

Website |  + posts
Share This Article