Kesi dhidi ya Gavana Mwangaza yaigia siku ya pili

Tom Mathinji
1 Min Read

Kikao cha kusikiliza hoja ya kumbandua Gavana wa Meru Kawira Mwangaza vinaingia siku ya pili leo Jumanne, katika bunge la Senate.

Wakati wa kikao cha kwanza siku ya Jumatatu, Mwangaza alikanusha mashtaka yote dhiki yake mbele ya Maseneta na bunge la kaunti ya Meru.

Mwangaza anakabiliwa na mashtaka ya kukiuka katiba, utumizi mbaya wa mamlaka na utovu wa maadili.

Hii ni mara ya tatu kwa Gavana huyo kukabiliwa na hoja ya kumuondoa mamlakani, mara ya kwanza ikiwa mwezi Disemba mwaka 2022 na mara ya pili mwezi Novemba mwaka 2023.

Zipporah Kinya, aliyewasilisha hoja hiyo, siku ya ya Jumatatu alielezea makosa ya Gavana huyo, huku akiitaka bunge la Seneti kumbandua.

Iwapo bunge hilo la Seneti litashikilia uamuzi wa bunge la kaunti ya Meru wa kumtimua Mwangaza, basi naibu wake atachukua wadhifa wa Gavana wa Meru.

Na iwapo Seneti haitampata na hatia, basi litamfahamisha spika wa bunge la kaunti ya Meru kuhusu uamuzi huo.

Share This Article