Kenya yalaani mashambulizi ya Marekani huko Mashariki ya Kati

Dismas Otuke
2 Min Read
Rais William Ruto.

Taifa la Kenya limelaani mashambulizi yaliyotekelezwa na Marekani kwa ushirikiano na Israel dhidi ya mataifa mbali mbali ya eneo la Mashariki ya Kati.

Katika taarifa, Rais William Ruto alitaja mashambulizi hayo dhidi ya Muungano wa Milki za Kiarabu, Qatar, Saudi Arabia, Iraq, Oman, Kuwait, Jordan na Bahrain kuwa tishio kubwa kwa amani na usalama kimataifa.

“Ni dhahiri kwamba kufanya mgogoro huu kuwa wa kikanda kunatishia pakubwa amani na usalama wa kimataifa” alisema kiongozi wa nchi katika taarifa hiyo.

Ruto alisema pia kwamba katika wakati huu muhimu na hatari katika historia ya ulimwenu, mashirika endelevu ya kimataifa yanasalia kuwa mifumo muhimu katika kutatua mgogoro unaojiri katika eneo la Mashariki ya Kati.

Rais alimaliza taarifa yake fupi kwa kuhimiza mazungumzo ya wadau kadhaa kwa lengo la kukomesha mgogoro huo.

Iran imekuwa ikishambuliwa na Marekani na Israel tangu Jumamosi Februari 28, 2026, mashambulizi yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na viongozi wengine wakuu werikalini.

Jana Jumapili, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kupitia video kwamba Marekani itaendelea kushambulia Iran hadi itakapoafikia lengo lake.

Katika video hiyo, Trump alisema pia kwamba wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa kwenye mashambulizi hayo nchini Iran na huenda wakapata maafa zaidi kadri mashambulizi hayo yapotekelezwa.

Share This Article