Wahudumu wa afya nchini wametishia kugoma endapo serikali haitatimiza matakwa yao ndani ya siku 14 zijazo.
Vyama mbalimbali vinavyowakilisha wahudumu wa afya tayari vimetoa notisi za mgomo huku mgomo wa wastawishaji afya ya jamii( UHC), ukiingia mwezi wa tatu.
Baadhi ya matakwa ya wahudumu wa afya ni pamoja na; uainishaji wa mishahara na tume ya kuratibu mishahara SRC,kuajiriwa kwa kwa kandarasi za kudumu kwa wastawishaji wa afya ya jamii na kulipwa malipo yao ya kuhitimisha kandarasi kwa kipindi walichohudumu.
Mgomo huo unatarajia kulemaza huduma za afya hususan katika hospitali za umma kote nchini, ambazo hutegemewa sana na kina yahe.